Wednesday, January 23, 2013

KICHANGA CHATUPWA UWANJA WA MPIRA MALIMBE

Mtu asiyejulikana ametupa kichanga ambacho ambacho kilizaliwa kabla ya muda wake. kichanga hicho ambacho kinakisiwa kimezaliwa kikiwa na kati ya miezi saba na minane kimekutwa kimetupwa katika uwanja wa mpira Malimbe ulioko katika chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT) huko Malimbe jijini Mwanza.
Wachezaji wa mpira uwanjani hapo wakiwa katika mazoezi yao ya jioni wamekikuta kichanga hicho kimetelekezwa uwanjani hapo huku kikiwa kimefariki.
Mashuhuda wa tukio hilo wamepeleka lawama zao kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha SAUT kwa kuhusika na tukio hilo.
Mpaka ripota wa habari hizi anaondoka eneo la tukio jeshi la polisi alikuwa wamefika eneo hilo kuchukua mwili wa kichanga hicho na kuanza uchunguzi rasmi wa tukio hilo.